KIKOKOTOO
Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli amefanya mkutano Ikulu jijini Dar es salaam na wawakilishi wa wafanyakazi wa umma na sekta binafsi juu ya Kikokotoo cha mafao ya mstaafu.
Katika mkutano huo rais Magufuli amesema "mtu aliyetumikia taifa hadi kustaafu bila kufukuzwa anastahili pongezi kubwa hivyo lazima aheshimiwe"
Mhe. Rais amesisitiza kuwa kikokotoo cha 25% hata mawaziri hawatokubali baada ya ubunge wao wapewe asilimia 25, na zingine wapewe kidogo kidogo hadi mwisho.
Katika kuhitimisha hoja zake Rais Magufuli ameitaka mifuko yote ya hifadhi za jamii kutumia Vikokotoo vilivyopo hivi sasa hadi kumaliza kipindi cha mpito yaani adi mwaka 2023.
Maoni
Chapisha Maoni